Job Ndugai afariki dunia

DODOMA: SPIKA Mstaafu na aliyekuwa Mbunge wa Kongwa mkoani Dodoma, Job Ndugai amefariki dunia.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kitengo cha Mawasiliano na Elimu kwa Umma cha Ofisi ya Bunge, Ndugai amefariki dunia leo Agosti 6, 2025 jijini Dodoma.
“Kwa masikitiko makubwa, naomba kutoa taarifa ya kifo cha kiongozi wetu, mwanasiasa mkongwe na Spika Mstaafu wa Bunge, Mheshimiwa Job Yustino Ndugai kilichotokea leo jijini Dodoma.
“Natoa pole kwa familia ya Marehemu, ndugu, jamaa na wananchi wa Jimbo la Kongwa, Mwenyezi Mungu awape moyo wa uvumilivu na subira katika kipindi hiki kigumu.” amesema Spika wa Bunge na Rais wa Umoja wa Mabunge duniani, Dk. Tulia Ackson kupitia taarifa hiyo.
Aidha, ofisi ya Bunge kwa kushirikiana na Kamati ya Mazishi pamoja na familia ya marehemu inaratibu mipango ya mazishi na taarifa zaidi zitaendelea kutolewa.