SUA yaonesha umahiri kwenye kilimo mazao

MOROGORO: CHUO Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kimeibuka kidedea kwa kuwa Mshindi wa Jumla na Mshindi wa Kwanza katika kundi la Taasisi za Mafunzo na Utafiti katika Maonesho ya Nanenane Kanda ya Mashariki yamwaka huu ( 2025) yaliyofanyika mkoani Morogoro na unatokana na mchango wake mkubwa katika sekta ya kilimo nchini.

Akizungumza mara baada ya kupokea ushindi huo, Makamu wa Mkuu wa SUA, Profesa Raphael Chibunda, aliwapongeza wafanyakazi wa Chuo hicho kwa juhudi zao wanazozionesha .

Profesa Chibunda amesema kuwa ushindi huo umetokana na mchango wa Chuo Kikuu hicho katika kutoa elimu kwa jamii kupitia tafiti, teknolojia mbalimbali, na wataalamu wake bobezi wanaoleta chachu ya maendeleo katika sekta ya kilimo nchini.

“Mbali na mashamba darasa tunayotoa katika maonesho haya, SUA pia tuna ndege isiyo na rubani kwa ajili ya shughuli za kilimo hasa kwenye umwagiliaji wa mbolea na dawa” amesema .

Profesa Chibunda pia amesema Chuo kina maabara inayotembea ambayo imekuwa msaada mkubwa katika kutatua changamoto za magonjwa kwa mifugo, wanyamapori na binadamu.

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu hicho alitoa rai kwa jamii kuendelea kuitumia SUA ili kujifunza kupitia tafiti na ushauri wa kitaalamu kwa lengo la kuwa na kilimo chenye tija na kilimo biashara kwa maslahi ya taifa.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Taasisi ya Elimu ya Kujiendeleza (ICE) na Mtafiti kutoka SUA, Dk Devotha Mosha, aliishukuru Menejimenti ya Chuo kwa kuwezesha ushiriki mzuri kwenye maonesho pamoja na kusisitiza jamii kuendelea kukitumia Chuo Kikuu hicho ili kufanikisha maendeleo katika kilimo na maisha kwa ujumla.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button