Joto kali Ulaya laua watatu

LONDON, UINGEREZA : WATU  watatu wamefariki dunia na maelfu kulazimika kuyahama makazi yao kutokana na mioto ya nyika inayosababishwa na wimbi la joto kali linaloikumba kusini mwa Ulaya.

Watu wawili walipoteza maisha nchini Uhispania na mmoja nchini Montenegro, huku tahadhari ya joto la kupindukia ikitolewa nchini  Italia, Ufaransa, Uhispania, Ureno na mataifa ya Balkan. Katika baadhi ya maeneo, joto linatarajiwa kufikia nyuzi 40 za Selsiasi, hali inayoongeza hatari ya kuendelea kushika kasi kwa mioto hiyo.

Mtafiti wa hali ya hewa kutoka Chuo Kikuu cha Reading, Uingereza, Akshay Deoras, amesema wimbi hilo la joto ni ishara nyingine ya mabadiliko ya tabianchi, lakini akionya kuwa bado watu wengi hawatilii maanani tishio hilo. SOMA: Moto waua wafanyikazi 40 wa India huko Kuwait

 

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button