Moto waua wafanyikazi 40 wa India huko Kuwait

KUWAIT – Takriban Wahindi 40 walikufa wakati moto mkubwa ulipozuka katika jengo la makazi katika mji wa Mangaf huko Kuwait siku ya Jumatano, Wizara ya Mambo ya Nje ya India imesema.

Waziri Mkuu wa India Narendra Modi alisema ubalozi wa nchi hiyo huko Kuwait unafuatilia kwa karibu hali hiyo na kufanya kazi na mamlaka za mitaa kusaidia wale walioathiriwa na “ajali hiyo ya kusikitisha.”

“Mawazo yangu ni kwa wale wote ambao wamepoteza wapendwa wao wa karibu. Ninaomba kwamba waliojeruhiwa wapone mapema,” Modi aliandika katika chapisho kwenye X (zamani Twitter).

Waziri wa Jimbo la India Shri Kirti Vardhan Singh alisafiri kwenda Kuwait ili kupata urejeshaji wa mapema wa mabaki ya waathirika, na pia kuhakikisha kuwa waliojeruhiwa wanapata msaada wa matibabu, wizara ya mambo ya nje ilisema.

Video zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii zinaonyesha miali ya moto ikiteketeza sehemu ya chini ya jengo la gorofa sita iliyokuwa na wafanyakazi, na moshi mzito, mweusi ukitanda katika gorofa za juu.

Idadi ya jumla ya waliofariki kutokana na moto huo imefikia 53, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Kuwait iliripoti, na kuongeza kuwa “wengine wengi” wamejeruhiwa katika ajali hiyo. Waziri wa Afya wa Kuwait Ahmad Al-Awadhi, amesema watu 56 walilazwa hospitalini.

SOMA: Ukraine yatawala mkutano wa G7 Italia

Emir Sheikh Meshal al-Ahmad al-Sabah ameagiza uchunguzi ufanyike kuhusu chanzo cha moto huo akisisitiza kuwa yeyote atakayebainika kuhusika atawajibishwa.

Naibu waziri mkuu wa kwanza wa Kuwait na waziri wa mambo ya ndani, Sheikh Fahad Yousuf Al-Sabah, aliahidi kuwa majengo ya ghorofa yatakaguliwa kwa ukiukaji “bila onyo” kufuatia tukio hilo.

Naibu waziri mkuu alishutumu wamiliki wa mali kwa uchoyo, akisema kuwa ukiukaji wa viwango vya ujenzi ndio uliosababisha janga la Jumatano.

Habari Zifananazo

Back to top button