Mgombea urais SRT awapa tahadhari wajumbe

ARUSHA: MGOMBEA wa nafasi ya Makamu wa Rais wa Shirikisho la Riadha Tanzania (SRT), Baraka Sulus amewaambia wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Shirikisho hilo kuwa hatma ya kukuza mchezo huo kurudi katika sifa za miaka ya nyuma iko mikononi mwao katika uchaguzi wa Agosti 16 mwaka huu.

Amesema ili kufanikisha hilo  wanapaswa kuhakikisha wanachagua viongozi wenye weledi, waadilifu na wenye mapenzi na mchezo huo vinginevyo utakufa.

Baraka ambaye ni mtoto wa mzee Elias Sulus aliyeongoza SRT katika miaka ya 1986 hadi 2006 kwa mafanikio amesema hayo jijini Arusha na kuongeza kuwa wajumbe ndio wenye maamuzi katika uchaguzi huo hivyo ni wajibu wao kuchagua viongozi wenye sifa.

Amesema na kusisitiza kwa kuwaomba wajumbe kuwa sio wakati wa SRT kuongozwa na viongozi wasiokuwa na sifa na kuliingiza Shirikisho hilo katika kashfa ya matumizi mabaya ya fedha na kuongoza bila kushirikisha wenzao kwani akichaguliwa atahakikisha halitakuwepo kwani atashirikisha uongozi kwa pamoja ili kuendeleza mchezo huo hapa nchini na nje.

Baraka ambaye ni wakili wa Mahakama ya Tanzania, Kamishna wa Viapo na Mthibitishaji wa Nyaraka za Umma amesema moja ya vipaumbele vyake iwapo atapatiwa riadha kuongoza shirikisho hilo ni pamoja na kuhakikisha anasimamia mikataba ya wazi ya SRT, mikoa na wanariadha kuhakikisha mikataba ya wanariadha inalindwa kisheria na kuwatumia ipasavyo wanariadha nyota wa zamani katika kuleta chachu ya maendeleo ya riadha nchini.

‘’Mchezo wa riadha ni moja ya mchezo unayoijengea sifa nchi katika miaka ya nyuma kwa baadhi ya wanariadha kuvunja rekodi zilizowekwa na wanariadha wa nje hivyo nikichaguliwa niyahakikisha hilo linarudi kama zamani kwa kushirikiana na kama tendaji itakayochaguliwa,’’alisema Sulus.

Naye Mgombea Urais wa SRT, Rogart Steven anaishukuru kamati ya uchaguzi ya shirikisho hilo kwa kumpitisha kuwa mmoja wa wagombea sita wa nafasi hiyo na aliwaomba wajumbe wa Mkutano Mkuu kutofanya makosa kuhakikisha wanamchagua yeye kuwa Rais wa Shirikisho hilo kwa kuwa ana uwezo wa kuongoza.

Steven ambaye ni Katibu wa RT Mkoa Arusha amesema kuwa hana maneno mengi ya kujieleza kwa kuwa wajumbe wa Mkutano huo wanajua vilivyo utendaji kazi wake uliotukuka uliojaa uadilifu na ushirikisha hivyo aliwaomba wamchagua yeye kuendeleza mchezo wa riadha nchini na sio vinginevyo.

Naye Mwenyekiti wa zamani wa RT mkoani Arusha, Wifredo Shahanga ambaye anagombea ujumbe wa Kamati Tendaji wa Shirikisho hilo yeye amesema familia ya riadha nchini inamjua katika utendaji kazi wake hivyo aliwakumbusha wajumbe kutosita kumchagua yeye kuliongoza shirikisho hilo katika kipindi kijacho.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button