Ushuru Marekani, Brazil yachukua hatua

BRAZIL : SERIKALI ya Brazil imezindua mpango wa kuyaunga mkono makampuni ya ndani yaliyoathiriwa na ushuru wa asilimia 50 uliotangazwa na Rais Donald Trump kwa bidhaa kadhaa za nchi hiyo.

Rais wa Brazil Luiz Inacto lula da Silva ameelezea mpango huo wa kifedha wenye thamani ya dola bilioni 5.5, kama hatua ya kwanza ya kusaidia wauzaji bidhaa wa ndani. SOMA: BRICS yapingana na ushuru wa Trump

Kiongozi huyo wa mrengo wa kushoto, ambaye ushawishi wake umepanda tangu ushuru dhidi ya nchi yake kutangazwa, kwa mara nyingine alisema yeye na Trump hawajawahi kuzungumza, na kudai kuwa rais huyo wa Marekani hataki kufanya mazungumzo.

Mpango huo unatoa muda zaidi wa ulipaji kodi kwa kampuni zinazoathirika na ushuru wa Marekani, kutoa mikopo kwa makampuni madogo na ya kati hadi mwisho wa mwaka 2026, na bima kwa bidhaa ambazo tayari zimeagizwa.

 

 

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button