BRICS yapingana na ushuru wa Trump

BRAZIL : SERA mpya za ushuru zilizowekwa na Rais wa Marekani, Donald Trump, zimechukua nafasi kubwa katika ajenda ya mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje wa nchi za BRICS unaofanyika mjini Rio de Janeiro, Brazil.

Mkutano huo wa siku mbili unawakutanisha mawaziri wa mambo ya nje kutoka mataifa wanachama wa BRICSĀ  ikiwemo Brazil, Urusi, India, China na Afrika Kusini kwa lengo la kutafuta msimamo wa pamoja kuhusu mvutano wa kibiashara unaoendeshwa na Marekani.

Akizungumza katika mkutano huo, Waziri wa Mambo ya Nje wa Brazil, Mauro Vieira, amesema kuwa wakati huu ambapo dunia inakabiliwa na migogoro ya kibinadamu, mizozo ya kivita na kuyumba kwa hali ya kisiasa, ni muhimu kwa jumuiya ya BRICS kuimarisha mdahalo na mshikamano.

SOMA: BRICS kuwekewa vikwazo vya ushuru -Trump

Ameongeza kuwa katika mazingira haya ya changamoto za kimataifa, nafasi ya BRICS imezidi kuwa muhimu kwa ajili ya kulinda mfumo wa biashara wa pande nyingi na kuhimiza usawa wa kiuchumi duniani.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button