MAREKANI : RAIS mteule wa Marekani Donald Trump ametishia kutoza ushuru kwa asilimia 100 kwa muungano wa mataifa tisa ya BRICS iwapo yataunda sarafu pinzani dhidi ya dola ya Marekani.
Nchi zenye nguvu kubwa duniani China na Russia ni sehemu ya muungano wa Brics, pamoja na Brazil, India, Afrika Kusini, Iran, Misri, Ethiopia na Umoja wa Falme za Kiarabu.
Wakati akifanya kampeni zake, Turmp alitoa vitisho kwa mataifa ya muungano wa Brics kuwatoza ushuru mkubwa ili kulinda thamani ya dola ya Marekani.
Hatahivyo, wanasiasa wakuu nchini Brazil na Urusi walipendekeza kuunda sarafu ya Brics ili kupunguza utawala wa dola ya Marekani katika biashara ya kimataifa.