Watoa misaada 383 wauawa 2024

NEW YORK, MAREKANI: UMOJA wa Mataifa umesema wafanyakazi 383 wa mashirika ya kutoa misaada waliuawa katika maeneo ya mapigano duniani mwaka 2024.
Kwa mujibu wa Mratibu Mkuu wa misaada ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa, Tom Fletcher, idadi hiyo ni onyo kwa jamii ya kimataifa kuhusu haja ya kuwalinda raia pamoja na wale wanaojitolea kuwasaidia.
Katika taarifa yake ya kuadhimisha Siku ya Misaada ya Kibinadamu Duniani inayofanyika kila Agosti 19, Fletcher alisema mashambulizi dhidi ya wahudumu wa misaada ni kielelezo cha kutowajibika na “aibu kwa dunia.” SOMA: Mashambulizi ya anga yaua watu 30
Takwimu za Kanzidata ya Usalama wa Wahudumu wa Misaada zinaonyesha vifo viliongezeka kutoka 293 mwaka 2023 hadi 383 mwaka 2024, ambapo zaidi ya 180 kati ya hao waliuawa katika Ukanda wa Gaza.



