Mashambulizi ya anga yaua watu 30

GAZA, PALESTINA:TAKRIBAN watu 30 wameuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa kufuatia mashambulizi ya anga yaliyofanywa na Jeshi la Israel katika Ukanda wa Gaza, usiku wa kuamkia leo.

Kwa mujibu wa mashahidi na wafanyakazi wa Hospitali ya Nasser, watu wasiopungua 10 waliuawa na zaidi ya 50 kujeruhiwa katika shambulio lililotekelezwa kwenye hema la wakimbizi wa ndani katika eneo la Al-Mawasi, kitongoji cha Khan Younis.

Ripoti zinaeleza kuwa miongoni mwa waliouawa, watu sita walikuwa wa familia moja. Katika mashambulizi mengine yaliyotokea awali katika maeneo ya kaskazini mwa Gaza, watu 17 walipoteza maisha, akiwamo Mkurugenzi wa Hospitali ya Indonesia pamoja na familia yake nzima.

Hadi sasa, Jeshi la Israel halijatoa tamko lolote rasmi kuhusu mashambulizi hayo au idadi ya vifo vilivyosababishwa.Mashambulizi haya yanaendelea kuzua wasiwasi mkubwa katika jumuiya ya kimataifa kuhusu hali ya kibinadamu nchini Palestina, huku idadi ya waathirika ikiendelea kuongezeka.

SOMA: Wapalestina 56 wauawa Gaza

Habari Zifananazo

Back to top button