Kiza Mayeye atwaa fomu ubunge Kigoma Kaskazini

KIGOMA: Mgombea ubunge wa Chama Cha ACT Wazalendo, Kiza Mayeye amechukua fomu kutoka ume huru ya Taifa ya uchaguzi (INEC) ili kugombea ubunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini ikiwa ni muendelezo wa Uchaguzi Mkuu wa Rais, wabunge na madiwani unaotarajia kufanyika kwenye Oktoba mwaka huu.

Mayeye amechukua fomu kutoka kwa msimamizi wa uchaguzi wa INEC katika Jimbo la Kigoma Kaskazini mkoani Kigoma, Linus Sikainda huku akieleza kuwa ameamua kuchukua fomu kugombea ubunge katika jimbo hilo ili kuwa sauti ya wananchi wa jimbo hilo katika kusimamia mahitaji muhimu ya kibinadamu ya wananchi hao.

Mgombea huyo amesema kuwa miongoni mwa mambo ambayo atayapa kipaumbele akichaguliwa kuwa mbunge wa jimbo hilo ni pamoja na kuitaka serikali kuimarisha upatikanaji wa huduma za afya sambamba na uwepo wa bima ya afya kwa wote na upatikanaji wa huduma bora ya elimu ikiwemo kuhakikisha serikali inaajiri walimu wa kutosha badala ya wazazi kutoa fedha kwa ajili ya kuajili walimu wa kujitolea.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button