Dk. Mwigulu akagua uharibifu wa vurugu

WAZIRI Mkuu, Dk. Mwigulu Nchemba, leo Novemba 24, 2025, amekagua miundombinu na mali zilizoharibiwa kufuatia vurugu zilizotokea Oktoba 29, 2025 jijini Dar es Salaam. Ziara hiyo imelenga kujionea uharibifu uliotokea katika huduma za umma na biashara binafsi na kutoa maelekezo ya kurejesha hali ya kawaida.

Katika ziara hiyo, Dk. Mwigulu ametembelea Kituo cha Mafuta cha Puma kilichopo Kimara Baruti, vituo vya mwendokasi vya Kimara Korogwe na Kimara Mwisho, pamoja na Kituo cha Mafuta cha Rupees kilichopo Kimara Stop Over. SOMA: Vyombo vya habari vizingatie weledi kulinda amani, uzuri wa Tanzania

Waziri Mkuu Dk. Mwigulu pia amezungumza na wahusika katika maeneo hayo ili kupata taarifa za kina kuhusu athari za kiuchumi na athari za utoaji huduma kwa wananchi.

Ameongezea kuwa Serikali itahakikisha hatua madhubuti zinachukuliwa ili kurejesha vifaa, miundombinu na huduma zilizokatizwa, sambamba na kuhakikisha usalama na utulivu unaendelea kudumishwa katika jiji la Dar-es-salaam .

 

 

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button