Hasham achukuwa fomu Ulanga

MOROGORO: Aliyekuwa mbunge wa jimbo la Ulanga kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Salim Alaudin Hasham ameahidi ahadi ujenzi wa hospitali ya wilaya sambamba na skimu za umwagiliaji ili kuongeza uzalishaji wa chakula kupitia kilimo cha umwagiliaji.

Ahadi hizo amezitoa leo wakati alipofika kwenye ofisi ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (INEC ) kwa ajili ya kuchukuwa fomu ili kuomba nafasi ya ubunge wa jimbo hilo.

“Nitakwenda kuwasemea wanaulanga kwa kuiomba serikali iweze kutujengea hospitali ya wilaya itakayokidhi ongezeko la wananchi, ujenzi wa skimu za umwagiliaji katika maeneo ya Lupiro,Lukande, Iyoga na Minepa pamoja na ujenzi wa barabara kutoka Ifakara hadi Mahenge kwa kiwango cha lami.”amesema Salim.

Salim amechukua fomu hiyo leo agosti 26, na kuahidi kuisimamia na kuitekeleza ilani ya CCM endapo atapata nafasi hiyo.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button