Magembe achukua fomu kumrithi Kalemani

Mgombea Ubunge wa Jimbo la Chato Kasikazini aliyepitishwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) Coronel Lucas Magembe amechukua fomu rasmi ya kuingia kwenye kinyang’anyiro cha uchaguzi mkuu chini ya usimamizi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi Nchini (INEC).

Akizungumza muda mchache baada ya kuchukua fomu katika ofisi ya msimamizi wa uchaguzi jimbo la Chato Kasikazini, Magembe amesema kuwa dhamira yake kuwania nafasi ya ubunge kupitia CCM ni kutatua kero za wananchi endapo wananchi watamchagua kuwa mbunge wa Jimbo hilo.

Aidha Magembe amewashukuru wajumbe na wanachama wa CCM jimbo la Chato Kasikazini pamoja na Kamati Kuu ya CCM Taifa kwa kumpa ridhaa na kumuon kuws anafaa kuipeperusha bendera ya CCM katika nafasi ya ubunge

Ifahamike kuwa kabla ya kupitishwa na Kamati Kuu ya CCM Taifa, Magembe alitangazwa kuwa mshindi wa kura za maoni kwa katika uchaguzi wa ndani wa CCM baada ya kupata kura 4, 298 akifuatiwa na aliyekuwa mbunge wa Jimbo la Chato Dkt Medard Kalemani aliyepata kura 1,390.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button