Serikali imefanya makubwa – Mathayo

SAME: MBUNGE mteule wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ,Jimbo la Same Magharibi ,David Mathayo amesema serikali imefanya makubwa katika jimbo hilo katika kuleta miradi ya maendeleo hivyo ni wakati wa wananchi kulipa fadhila kwa kuwaunga mkono wagombea wa chama hicho.

Mathayo amesema hayo wakati akirudisha fomu katika ofisi ya Tume Huru ya Uchaguzi (INEC) Jimbo la Same Magharibi leo na kusema mwishoni mwa mwezi Oktoba ni siku ya upigaji kura kwa vyama vyote katika nafasi ya urais, ubunge na udiwani na jukumu pekee kwa wananchi wa jimbo hilo ni kumuunga mkono Rais, yeye na madiwani wa chama tawala.

Ameishukuru Kamati Kuu ya Taifa ya CCM kwa kuwa na imani naye na hatimaye kumpendekeza kuwani tena nafasi hiyo katika miaka mitano ijayo na kusema sasa atatumia gia kubwa kusukuma maendeleo katika jimbo hilo ili kuendelea kuijenga imani chama kuwa hawakufanya makosa kumpendekeza yeye kuwania tena kiti hicho ubunge katika Jimbo la Same Magharibi.

Amesema waliowania nafasi hiyo ndani ya chama katika michakato ya ndani ya chama sio kuwa hawana sifa kwa kuwa hawakupendekezwa hapana kwani CCM ina hazina kubwa ya viongozi wenye weledi ,uadilifu ,uongozi bora na ushirikishaji wa kila jambo na yeye ni moja ya hazina hiyo na ndio maana amependekezwa na chama.

”Ninawaomba wale wasiopendekezwa kumuunga mkono katika kampeni kwa kuwa chama ni cha wote na wala sio cha mtu mmoja kwa kuwa mwaka huu atakuja na gia kubwa katika kusuka maendeleo katika Jimbo la Same Magharibi”alisema Mathayo

Naye Abdull Mwanga mkazi wa Jimbo la Same Magharibi  aliwataka wana CCM wa jimbo hilo kuwa wamoja na kuhakikisha chama hicho kinapata kura za kishindo kwa urais,ubunge na madiwani ili kuuonyesha umma kuwa jimbo hilo ni la chama tawala na sio vinginevyo.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button