Tanzania kuwa kitovu uchumi wa kijani wa nishati safi

KATIKA kipindi kifupi kijacho Tanzania itakuwa kitovu cha uchumi wa kijani hususani katika utengenezaji wa magari ya umeme, betri za magari, nishati safi na vifaa vya kielektroniki, imeelezwa.

Tanzania itakuwa kitovu cha uchumi wa kijani kutokana na mkakati wake wa kuhakikisha rasilimali madini zinaongezwa thamani ndani ya nchi na kufaidisha Watanzania kupata ajira, kuchangia kodi na mapato ya serikali.

Kauli hiyo ilitolewa na Waziri wa Madini, Anthony Mavunde wakati akiweka jiwe la msingi la Kiwanda cha Kusafisha na Kusindika Madini ya Nikeli na Shaba kinachojengwa na Kampuni ya Zhongzhou Mining, eneo la Zamahero, Wilaya ya Bahi mkoani hapa.

SOMA: Tanzania yanadi fursa za uwekezaji mnyororo madini muhimu London

“Ujenzi wa kiwanda hiki ni uthibitisho kuwa dhamira ya kuongeza thamani madini nchini, tunataka kuona Tanzania ikibadilika na kuwa taifa linalozalisha bidhaa zenye thamani kubwa kwenye soko la dunia la bidhaa teknolojia,” alisema.

Mradi huo utekelezaji wake ni kwa maelekezo ya Rais Samia Suluhu Hassan kwamba madini yanayochimbwa hapa nchini yaongezewe thamani ndani ya nchi na kuuza bidhaa ya mwisho ya badala ya madini ghafi.

Mradi huo wa Dola za Marekani milioni 15 utakapokamilika utazalisha takribani tani 200,000 za nikeli na shaba
kwa mwaka, kuajiri zaidi ya Watanzania 200 hadi 230 na kuchangia kodi na mapato mengine ya serikali.

“Uwekezaji huu ni kielelezo cha mafanikio ya serikali katika kufanikisha dira ya uchumi wa viwanda na uongezaji thamani madini kama ilivyoelekezwa na Ilani ya CCM ya mwaka 2020– 2025,” alisema.

Sera ya Madini ya mwaka 2009 inaelekeza kuyaongezea thamani madini ndani ya nchi.

“Hivi sasa Tanzania tuna viwanda vinane vya kusafisha madini ya dhahabu lakini viwanda vya kuongezea thamani madini ya metali tunavyo tisa, Mkoa wa Dodoma peke yake tunavyo vitano,” alisema.

Naye Kamishna wa Madini, Dk Abdulrahman Mwanga alisema uwekezaji kwenye miradi ya kuongeza thamani kunaifanya nchi kujenga msingi imara wa ajira, mapato, na uchumi shindani kimataifa na kufikia lengo la ujenzi wa Tanzania ya uchumi.

Mkurugenzi wa Kampuni ya Zhongzhou Mining, Lee Zhong Liang amemhakikishia Mavunde kuwa kampuni yake itaendeleza uhusiano mwema na serikali pamoja wananchi wanaozunguka mradi huo.

Katibu Tawala Wilaya ya Bahi, Mwanamvua Muyongo alisema uwepo wa kiwanda hicho katika wilaya hiyo utasaidia kuiweka katika ramani ya wazalishaji wa bidhaa muhimu za kiteknolojia pamoja na kuboresha maisha ya watu wa hapa kupitia ajira rasmi na zisizo za moja kwa moja.

Habari Zifananazo

2 Comments

  1. I make $88 an hour to work part time on a laptop. I never thought it was possible but my closest friend easily made $18,000 in 3 weeks with this top offer and she delighted me to join. .Visit the following article for new information on how to access…….
    .
    HERE——————————————⊃⫸ http://Www.Cash43.Com

  2. Some genuinely fantastic blog posts on this site, regards for contribution. “We are always in search of the redeeming formula, the crystallizing thought.” by Etty Hillesum.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button