Uwanja wa kisasa wakamilika Zanzibar

Moja ya ahadi muhimu katika Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuhusu uboreshaji wa miundombinu ya michezo visiwani Zanzibar imetimia, baada ya kukamilika kwa ujenzi wa kiwanja cha kisasa cha michezo katika eneo la Kitopeni, Wilaya ya Kaskazini B, Unguja.
Akizungumza wakati wa ziara ya kutembelea miradi ya maendeleo ya CCM, Katibu wa Siasa na Uenezi wa Wilaya hiyo, Hamada Shaha Vuai, alisema kuwa viwanja 17 vya michezo vilivyopangwa kwenye Ilani ya uchaguzi sasa vinaendelea kukamilika, na Kitopeni ni miongoni mwa vilivyokamilika kwa ubora wa hali ya juu.
“Watoto wanayo haki ya kusoma, lakini pia wanapaswa kuwa na maeneo ya kuchezea ili kukuza vipaji vyao. Kiwanja hiki cha Kitopeni kimejengwa mahsusi kwa ajili hiyo,” amesema Shaha Vuai.
Uwanja huo wa kisasa, wenye nyasi bandia, umejengwa kwa kipindi cha miezi sita kuanzia Februari mwaka huu na umegharimu takriban Shilingi Bilioni 5. Kwa mujibu wa Mhandisi Feisa Sule, ambaye ni msimamizi wa mradi, uwanja huu hautatumika tu kwa mechi bali zaidi kwa mazoezi na kukuza vipaji vya watoto.
“Ni uwanja wa mazoezi kwa michezo mbalimbali kama vile soka, netiboli, mpira wa wavu na mpira wa kikapu,” amesema Mhandisi Sule.
Mradi huu ni sehemu ya mkakati wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kupitia CCM kuinua sekta ya michezo, hasa kwa watoto na vijana, ili waweze kushindana kitaifa na hata kimataifa.
Katibu wa Siasa Vuai alihitimisha kwa kusema kuwa miradi hii ya maendeleo ni uthibitisho wa utekelezaji wa ahadi za CCM kwa wananchi na inalenga kuleta mabadiliko chanya kwa vijana wa Zanzibar.
JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… You can earn from 6000-12000 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good earning opportunity. tab for more detail thank you……..
HERE——————————————⊃⫸ http://Www.Cash43.Com