Watakiwa kujadiliana na wazazi kujiunga Mr Right

VIJANA wanaotamani kushiriki katika shindano la kutafuta wapenzi lijulikanalo kama Hello Mr. Right wametakiwa kuzungumza na wazazi wao mapema kabla ya kujiandikisha, ili kuhakikisha wanashiriki kwa uwazi na uhalali wa kijamii na kifamilia.

Akizungumza kuhusu msimu mpya wa shindano hilo, Godfrey Lugalabamu maarufu kama Mc Gara B, amesema Hello Mr. Right msimu wa saba utakuwa wa kipekee na wenye msisimko wa aina yake.

“Msimu huu washindi watafungwa ndoa rasmi. Tunatarajia kuona watu wakipendana kweli, wakitimiza vigezo, na kisha sisi tutashughulikia kila kitu kuhusu harusi yao,” amesema Gara B.

Ameongeza kuwa amerudi rasmi kama mmoja wa waendeshaji wa kipindi hicho baada ya kupumzika msimu uliopita, kufuatia maombi kutoka kwa mashabiki.

“Nimekuwa sehemu ya Hello Mr. Right tangu msimu wa kwanza. Mashabiki walisisitiza nirejee, na sasa narudi kwa kishindo, tukalete mahusiano mapya yenye matumaini,” amesema kwa kujiamini.

Kwa upande wake, Maimartha Jesse, mmoja wa watangazaji wa kipindi hicho, alisisitiza umuhimu wa mawasiliano kati ya washiriki na familia zao.

“Tunahimiza vijana wazungumze na wazazi kabla ya kujiunga, kwani lengo letu ni kuunganisha watu wanaopendana na hatimaye kuingia kwenye ndoa. Pia tunazingatia afya za washiriki kabla ya kuwaruhusu kuingia kwenye mahusiano ya kudumu,” amesema Maimartha.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button