Wafugaji wamuahidi raha Dk Samia

DODOMA; CHAMA cha Wafugaji Tanzania kimeahidi kutiki kwa mgombea urais kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Rais Samia Suluhu Hassan katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29 mwaka huu na kubainisha sababu za kufanya hivyo ikiwemo kuimarisha utulivu kati ya wafugaji na wakulima.
Mwenyekiti wa Chama cha Wafugaji, Murida Mshota alisema Rais Samia ametatua mgogoro wa ardhi hali iliyochangia utulivu kati ya wafugaji na wakulima kwa kutenga ekari milioni 3.46 za ufugaji na kuwapatia ruzuku ya Sh bilioni 210 katika kipindi cha miaka mitano.
“Katika kipindi chake pia tumepatiwa madawa ya kuogeshea mifugo, kujengewa majosho 754 yenye thamani ya shilingi bilioni 16 na kupatiwa madume kwa ajili ya mbegu.
” Pia kupitia programu ya ‘Tupendane’ imeleta utulivu katika Wilaya ya Mvomero na Kilosa, nikuhakikishie wafugaji hawataki migogoro, siku zote matajiri hawapendi migogoro. Tunashukuru kazi kubwa imefanyika, sisi wafugaji tutampa kura za kutosha ili andeleze mazuri aliyoyaanza,” amesema Mwenyekiti huyo.
Mshota alisema sababu nyingine ya kumpigia kura mgombea wa CCM ni kutokana na Serikali ya Rais Samia kuongeza maeneo ya ufugaji kutoka ekari milioni 3 hadi ekari milioni 6 hatua itakayowafanya wafugaji wasiwe na migogoro ya wafugaji na wakulima.
Alisema sababu myingine ni hatua ya serikali kutoa chanjo ya ruzuku mifugo kwa mifugo yote.
Pia alisema Serikali ya Rais Samia imeweza kuwajengea majosho 754 yenye thamani ya Sh bilioni 16 katika maeneo mbalimbali ambayo yamesaidia kuondoa magonjwa kwa mifugo.
Alisema amewapatia madawa ya mifugo lita laki 4 katika halmashauri 180 na madume 560 ambayo yamesambazwa katika halmashauri 8.
Akiwa katika kampeni katika Mkoa wa Morogoro, Rais Samia aliahidi kuongeza kasi ya upangaji matumizi ya ardhi katika sehemu ya ekari 53,476 ambazo serikali ilifuta umiliki wake kutokana na kutoendelezwa, hatua ambayo itasaidia kuondoa migogoro ya wafugaji na wakulima.
Alisema mpaka sasa zaidi ya ekari 21,000 zimepimwa na kugawanywa katika matumizi ya makazi, uwekezaji, kilimo, ufugaji na vikundi 186 kutoka vijiji 11 vya wilaya Mvomero.
PATA HABARI YA WWE MILIKI KIWANJA CHA KIWANDA PAMOJA NA £56,565,656,000 ONLINE LIVE HAPA + UCHAGUZI UKIISHA UTAGAWA KWA WATANZANIA £56,565,656,000 /56,000,000 maana tumekukabidhi NYOTA Yetu YA KUPATA HELA
PAMOJA NA bonanza la “We JuDGE….”
https://youtube.com/shorts/_jB1m_sfFuM?si=wSugXDCDnASW1bK6