Wasanii waipamba Dar, uzinduzi wa Chrome

DAR ES SALAAM: ULIKUWA ni usiku ambao kila mwana Dar es Salaam alitamani kuushuhudia namna wasanii na wabunifu walivyowasha moto viwanja vya Tanganyika Packers Kawe, usiku wa Agosti 30,2025.
Chino Wanna Man, D Voice, ni miongoni mwa wasanii waliolitawala jukwaa katika tukio la uzinduzi wa kinywaji cha Chrome.
Aidha, mbunifu wa mitindo, Audrey Erasrus ni miongoni mwa waliohudhuria uzinduzi wa kinywaji hicho kutoka Kampuni ya Seregenti Breweries.
Mara baada ya tukio hilo msanii huyo aliimbia HabariLeo kuwa: “Jukwaa hili limekuwa msaada mkubwa kwetu, nimepata nafasi ya kukutana watu na kutambulisha kazi zangu”.
Msanii mwingine, Simba Lameck alisema “Uzinduzi huu umenipa nafasi ya kuonesha ubunifu wangu na kupata wateja”.

Kwa upande wa Meneja wa Habari SBL, Gwamaka Mwankusye alisema Chrome inatoa hadithi ya ustahimilivu na mafanikio kwa kila kijana Mtanzania.
“Si kinywaji tu, mwamko mpya kusherehekea mwamko wa kazi na mafanikio.



