IATF2025 kukutanisha wafanyabiashara, wawekezaji

ALGIERS, Algeria: Wakuu wa nchi na serikali, wafanyabiashara na wawekezaji, wajasiriamali na wabunufu kutoka mataifa mbalimbali Afrika na ulimwenguni wanakutana leo kwa ajili ya maonesho makubwa ya nne ya kibiashara Afrika (IATF2025) yanayowaleta pamoja wageni zaidi ya 35,000.

Rais wa Algeria, Abdelmadjid Tebboune anatarajiwa kufungua maonesho hayo ambayo yanaratibiwa na Benki ya Uagizaji wa Bidhaa za Kiafrika (Afreximbank), Tume ya Umoja wa Afrika (AUC) na Sekretarieti ya Nchi Wanachama wa Mkataba wa Eneo Huru la Biashara la Afrika (AfCFTA).

Mkutano huo wa siku saba unaoanza leo Alhamis Septemba 4 hadi 10 unafanyika katika Mji Mkuu wa Algeria, Algiers na wageni kutoka mataifa 140 wakiwemo wakuu wa nchi na serikali wamewasili.

Baadhi ya viongozi ambao wamefika na wanatarajiwa kushiriki hafla ya ufunguzi ni pamoja na Rais wa zamani wa Nigerian na Mwenyekiti wa Baraza la Ushauri la IATF, Olusegun Obasanjo, Rais wa zamani wa Niger, Mahamadou Issoufou, Rais wa Sahrawi, Brahim Ghali, na viongozi wengine.

Mikataba yenyethamani ya zaidi ya Dola bilioni 44 inatarajiwa kusainiwa. Maonesho ya mwaka huu yatapambwa na siku ya kinataifa ya Diaspora kusherehekea uhusiano wa bara na Diaspora wake, Jukwaa la uwekezaji la Algeria, siku ya uvumbuzi na viwanda vya Afrika na Maonesho ya magari ya Afrika, teknolojia, kilimo na fedha.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button