Stars yawaduwaza Congo Brazzaville

CONGO BRAZZAVILLE: TIMU ya soka ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ imefungana bao 1-1 na Congo Brazzaville katika mchezo wa kuwania kufuzu fainali za Kombe la Dunia mwaka 2026.

Mchezo huo ulimaliizika muda mfupi uliopita nchini Congo Brazzaville, ambapo wenyeji walikuwa wa kwanza kupata bao dakika ya 68 mfungaji akiwa Dechan Moussavou, huku wenyeji wakiamini wangeibuka na ushindi, lakini Selemani Mwalimu ‘Gomes’ aliisaiwazishia Staras dakika ya 84.

Kutokana na matokeo hayo Stars inaendelea kushika nafasi ya pili kwenye Kundi E ikiwa na pointi 10 kwa michezo sita, nyuma ya vinara Morocco wenye pointi 15 kwa michezo mitano.

Congo Brazzaville yenyewe inashika nafasi ya tano ikiwa na pointi moja kwa michezo sita, baada ya kupoteza michezo yote mitano ya mwanzo.

Habari Zifananazo

9 Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button