Waamuzi kutoka nje waendelee kuchezesha Yanga, Simba

HISTORIA iliandikwa Juni 25, mwaka huu katika soka la Tanzania kwa waamuzi kutoka Misri kuchezesha mechi ya watani wa jadi, Yanga na Simba.
Mwamuzi Amin Mohamed Omar alichezesha mechi hiyo akisaidiwa na Mahmoud Abo El Regal kama mwamuzi msaidizi namba moja na Samir Mohamed ambaye alikuwa msaidizi namba mbili, wote kutoka Misri.
Ahmed Mahrous naye kutoka Misri alikuwa ofisa wa nne wa kigeni katika mchezo huo. Mtathmini waamuzi ni Alli Mohamed kutoka Somalia.
SOMA: Mechi ya Simba vs Yanga yasogezwa mbele
Kamishna wa mchezo huo uliochezwa majira ya saa 11:00 jioni katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam alikuwa Salim Singano, kutoka Tanzania.
Uamuzi huo ulifanywa na Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara (TPLB) kutaka haki ionekane kutendeka na mshindi halali apatikane.
Na kwa namna moja au nyingine bila kujali kama kanuni ziliruhusu wakati ule kuleta waamuzi hao kutoka Misri ama la, lilikuwa jambo jema hasa ukichukulia historia ya mchezo huo ambao ulipaswa kuchezwa Machi 8 lakini ukaahirishwa na mamlaka za soka kwa kile ambacho Simba ilidai kuzuiwa kufanya mazoezi Uwanja wa Benjamin Mkapa siku moja kabla ya mchezo huo.
Mchezo huo ulikuwa wa kuamua bingwa wa Ligi Kuu Bara na ambao ulizusha mjadala mkubwa huku Yanga ikiweka msimamo wake wa kutocheza tena mchezo huo, ikishinikiza pamoja na mambo mengine wapewe pointi tatu, wakiamini wapinzani wao Simba waligomea kwa makusudi Machi 8.
Hata hivyo, Yanga ilishinda mchezo huo kwa mabao 2-0 yaliyofungwa na kiungo Pacome Zouzoua kwa mkwaju wa penalti na mshambuliaji Clement Mzize.
Baada ya mchezo huo, mwitikio wa namna waamuzi wale wa Misri walivyochezesha ulikuwa mzuri kwamba walichezesha kwa haki na pengine ndiyo sababu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na kwa kutambua changamoto mbalimbali za waamuzi wa nyumbani, wakaamua kuweka kanuni itakayoruhusu waamuzi kutoka nje ya taifa hili kuchezesha mechi za Ligi Kuu.
Hivyo kuelekea mchezo wa Ngao ya Jamii, bila ya kubeza uwezo wa waamuzi wazawa, tunaamini TFF ina kila sababu kuleta waamuzi kutoka nje ya Tanzania kuchezesha mchezo huo wa Septemba 16, Uwanja wa Benjamin Mkapa.
TFF inapaswa kuleta waamuzi kutoka nje ya Tanzania kuchezesha mchezo huo wenye hisia kali miongoni mwa mashabiki wa soka, wa taifa hili ambao mapenzi yao ya dhati yamegawanyika kwa klabu kubwa hizo mbili, Yanga na Simba.
Lakini waamuzi wazawa wana kila sababu kuendelea kujifunza kutoka kwa waamuzi wa nje ya Tanzania na ambao wanaaminika sio tu na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) lakini pia hata Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) na kuwatumia kwenye mashindano mbalimbali makubwa kama wale kutoka Misri.
Kanuni inawaruhusu kuleta waamuzi hao kwani wameitunga wenyewe kulingana na hali halisi ya mpira wa Tanzania, lakini pia ukubwa na mazingira ya mchezo wenyewe ni sahihi kuendelea kuchezeshwa na waamuzi kutoka nje ya nchi mpaka pale waamuzi wa ndani watakapokuwa tayari.
I just got paid $22k working off my laptop this month!** And if you think that’s cool, my divorced friend has twin toddlers and made over $22620 her first month. details on this website**Want the secret?** Copy this Website and choose HOME TECH OR MEDIA…..
Here is I started_______ https://Www.CashHive1.Com