CHP yaitisha maandamano makubwa Istanbul

ISTANBUL, UTURUKI: CHAMA Kikuu cha Upinzani nchini Uturuki, Republican People’s Party (CHP), kimewataka wananchi na wakazi wa jiji la Istanbul kujitokeza kwa wingi leo Jumatatu, Septemba 8, 2025, kushiriki maandamano ya kupinga kile kinachoelezwa kuwa ni vitendo vya ukandamizaji wa sheria vinavyoendelea nchini humo.
Hatua hiyo inakuja wakati mamia ya wanachama wa chama hicho, akiwemo Meya wa Istanbul, Ekrem Imamoglu, wakiendelea kukamatwa, jambo linalodaiwa kudhoofisha maendeleo ya demokrasia nchini humo. SOMA: Korea Kusini kufanya maandamano kumpinga Rais Yoon Suk
Imamoglu, anayechukuliwa kuwa mpinzani mkuu wa kisiasa wa Rais Recep Tayyip Erdogan, alikamatwa mwezi Machi na tukio hilo liliibua maandamano makubwa zaidi ya barabarani kuwahi kushuhudiwa nchini humo katika kipindi cha muongo mmoja.



