Korea Kusini kufanya maandamano kumpinga Rais Yoon Suk

KOREA KUSINI : MAELFU ya watu nchini Korea Kusini wanatarajia kufanya maandamano kesho Jumamosi kumpinga Rais Yoon Suk Yeol.

Waandaaji wa maandamano hayo wamesema wanakadiria kuwa takriban watu 200,000 watashiriki maandamano hayo.

Polisi mjini Seoul imethibitisha kufanyika kwa maandamano hayo katikati mwa mji huo na eneo la Yeouido na kwamba imepanga kuweka vizuizi katika baadhi ya barabara.

Advertisement

Mwanzoni mwa wiki hii,Rais Yoon alitangaza sheria ya kijeshi kabla ya kulazimishwa kuubadili msimamo wake baada ya wabunge kupiga kura kuipinga sheria hiyo.

Hatahivyo, kambi ya upinzani imewasilisha hoja ya kumuondoa madarakani Yoon Suk Yeol ambayo inatarajiwa kupigiwa kura kesho Jumamosi, huku kiongozi wa chama cha Yoon akishinikiza rais huyo avuliwe madaraka. SOMA: Chama tawala kimemtaka Yoon Suk kujiuzulu