KOREA KUSINI : RAIS wa Korea Kusini, Yoon Suk Yeol ameendelea kushindikizwa kuondoka madarakani kufuatia tamko la kuitisha hali ya tahadhari nchini humo.
Mkuu wa chama tawala nchini Korea Kusini amesema Rais Yoon Suk Yeol anaweza kuwaingiza raia kwenye hatari kubwa endapo hakuondoshwa.
Han Dong-hoon anayeongoza chama cha People Power, amesema ikiwa Rais Yoon ataendelea kubakia madarakani, huenda hatua kali kama vile sheria ya matumizi ya nguvu za kijeshi, zinaweza kurejea, na hivyo kuiweka Jamhuri ya Korea na raia wake hatarini na kuomba madaraka ya kikatiba ya Rais Yoon yasimamishwe.
Han amesema Rais Yoon alikuwa ameagiza kukamatwa kwa wanasiasa wakubwa kwa madai kwamba wanapinga serikali. SOMA: Wabunge 108 wampinga Rais Yoon Suk