Wabunge 108 wampinga Rais Yoon Suk

KOREA KUSINI : MNADHIMU mkuu wa chama tawala nchini Korea Kusini Choo Kyung-ho amesema wabunge wa chama tawala 108 wamepanga kuungana kupinga kuondolewa madarakani kwa Rais Yoon Suk Yeol kufuatia kutangaza sheria ya kijeshi nchini humo.

Kambi ya upinzani imesema mchakato huo utafanikiwa endapo wabunge wanane kutoka chama tawala  watapitisha hoja hiyo. SOMA : Korea Kusini yapiga marufuku ulaji nyama ya mbwa

Kauli ya mnadhimu huyo wa chama tawala inakuja wakati tayari mkuu wachama hicho, Han Dong-hoon amemtaka Rais Yoon aondoke kwenye chama hicho na wamba chama chake hakitajaribu kumlinda rais huyo na sheria yake inayokwenda kinyume na sheria .

Advertisement

Tayari waziri wa ulinzi, Kim Yong-hyun, amejiuzulu na nafasi yake kuchukuliwa na balozi wa Korea Kusini nchini Saudi Arabia, Choi Byung-hyuk.