Nandy, Billnass waibua mshangao mitandaoni

KATIKA hali ya kushangaza na inayowashtua mashabiki wengi wa muziki wa Bongo Fleva, wanandoa maarufu William Lyimo ‘Billnass’ na mkewe Faustina Mfinanga ‘Nandy’ wameibua maswali mengi baada ya kuonekana kutofautiana kwa namna isiyo ya kawaida katika mitandao ya kijamii.

Taarifa zilizopo zinaeleza kuwa Nandy ameacha kumfuata mumewe kwenye mtandao wa Instagram na kufuta picha zote walizowahi kupiga pamoja. Hatua hiyo imefuatiwa na Billnass naye kuacha kumfuata Nandy. Tukio hilo limeacha maswali mengi miongoni mwa mashabiki, huku baadhi wakihisi huenda ni dalili za mgogoro wa kifamilia, na wengine wakidhani kuwa huenda ni kiki ya kisanii.

Kwa muda mrefu wawili hao walionekana kuwa mfano wa ndoa bora katika tasnia ya burudani, kiasi cha kupewa heshima ya kuwa walezi wa ndoa ya msanii Juma Jux na Priscilla.

Kwa sasa bado haijulikani chanzo cha hatua hiyo ya mitandaoni, huku mashabiki na wadau wa muziki wakiendelea kuwashauri na kuwaombea wenza hao waweze kushinda changamoto zinazowakabili. SOMA: Ndoto ya Nandy azae watoto 10

 

 

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button