Cuba yakosa umeme,wananchi waathirika

CUBA : KWA mara nyingine, taifa la Cuba limekumbwa na tatizo la kukatika kwa umeme nchi nzima kutokana na uchakavu wa miundombinu na uhaba wa mafuta kwenye mitambo ya kuzalisha nishati. Tukio hilo lililotokea Jumatano Septemba 10 ni la pili kwa mwaka huu na linafuatia matukio kama hayo mwaka jana.

Wizara ya Nishati na Madini imesema hitilafu hiyo imetokana na kuharibika kwa kinu kikubwa cha kuzalisha umeme nchini humo. Waziri Mkuu Manuel Marrero ametembelea kinu hicho na kuwaomba raia waendelee kuwa na imani na serikali, huku akiweka bayana changamoto za kiuchumi zinazoikumba nchi hiyo.

Vikwazo vya Marekani pia vimetajwa kama chanzo kikuu cha kuzorota kwa sekta ya nishati na uchumi wa Cuba. SOMA: Rais Mwinyi awasili Cuba

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button