Rais Mwinyi awasili Cuba

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Hussein Ali Mwinyi akiambatana na Mama Mariam Mwinyi pamoja na ujumbe wake amewasili nchini Cuba kuhudhuria Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa kundi la 77 na China (G77+China).

Mkutano huo utafunguliwa kesho ambapo Rais Mwinyi atamuwakilisha Rais Samia Suluhu Hassan.

Rais Dk Mwinyi amepokelewa na Balozi wa Tanzania, Humphrey Polepole na Maafisa wengine wa ubalozi wa Tanzania Havana, Cuba.

Advertisement

4 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *