Droni za Urusi zajadiliwa NATO

BRUSSELS, Ubelgiji : MABALOZI wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Kijeshi ya NATO wamekutana Jumatano Septemba 10 kujadili hatua za kuchukua baada ya droni za kijeshi za Urusi kuingia anga ya Poland. Kikao hicho kilichofanyika katika makao makuu ya NATO Brussels, kilikuwa chini ya Kifungu Namba 4 cha Mkataba wa NATO, kinachohusu mashauriano ya haraka endapo mwanachama atashambuliwa.

Waziri Mkuu wa Poland, Donald Tusk, alisema katika tukio hilo la Septemba 9, ndege za kijeshi za Poland zikisaidiwa na Uholanzi zilidungua baadhi ya droni hizo. Tukio hilo lilikuja siku tatu baada ya Urusi kufanya mashambulizi makubwa ya anga dhidi ya Ukraine tangu vita yao ianze. SOMA: Rais Samia awaita Poland kuwekeza Tanzania

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button