Starmer amtimua balozi kwa kashfa ya Epstein

LONDON: WAZIRI Mkuu wa Uingereza, Keir Starmer, amemfuta kazi Balozi wa Uingereza nchini Marekani, Peter Mandelson, kufuatia madai ya uhusiano wake wa karibu na mfanyabiashara aliyekuwa akikabiliwa na kesi za unyanyasaji wa kingono, Jeffrey Epstein.

Hatua hiyo imekuja baada ya kuvuja kwa barua pepe zinazodaiwa kuonesha Mandelson akiwasiliana mara kwa mara na Epstein. Katika mawasiliano hayo, Mandelson anadaiwa kuunga mkono utetezi wa Epstein na kueleza kuwa hukumu iliyokuwa ikimkabili ilikuwa batili na inapaswa kupingwa. SOMA: Samia ampongeza Waziri Mkuu mpya Uingereza

Waziri wa Mambo ya Nje, Stephen Doughty, aliliambia Bunge la Uingereza kuwa nyaraka hizo mpya zinaashiria ukaribu wa Mandelson na Epstein, kinyume na taarifa rasmi zilizotolewa na mamlaka wakati wa uchunguzi uliofanyika kabla ya uteuzi wa balozi huyo.

 

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button