JKCI yaadhimisha miaka 10 kwa bonanza la michezo

DAR ES SALAAM: TAASISI ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) imefanya bonaza katika kuadhimisha miaka 10 tangu kuanzishwa kwa taasisi hiyo yenye mafanikio makubwa Afrika Mashariki na Kati katika kutoa huduma za moyo.
Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa bonaza hilo liliofanyika jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI)Dk Peter Kisenge amesema bonaza hilo limeshirikisha wafanyakazi zaidi ya 687 wa taasisi hiyo.
“Tunaadhimisha mambo makubwa yaliyofanyika tangu 2015 imekubwa bora Afrika Mashariki na Kati katika kutoa matibabu ya tiba na upasuaji wa moyo .Ni taasisi pekee inayofanya upasuaji wa tundu dogo kwa Afrika Mashariki na Kati kwa kiasi kikubwa zaidi ya wagonjwa 3,000 kwa mwaka na upasuaji zaidi ya 800 kwa mwaka.
Dk Kisenge amesema mpaka sasa wagonjwa wa tudu dogo waliofanyiwa upasuaji ni 12,000 na oparation za kawaida 8,000.
“Hii ni kutokana na uwekezaji uliofanywa na serikali katika taasisi yetu uwekezaji wa vifaa abavyo ni vikubwa unaweza kulinganisha na nchi zilizoendelea kama Marekani na nchi za Asia,”amesisitiza.

Amesema wanamafaniko katika tiba utalii ambapo zaidi ya nchi 20 zinakuja JKCI kupata matibabu na wamewafikia wananchi kwa kuwafuata kwenye maeneo yao (outreach)zaidi 24,000.
“Leo tumeona tuadhimishe kwa michezo kwanza sisi kama madaktari tunaotibu moyo na magonjwa yasiyoambukiza tumeonesha kwa vitendo kufanya mazoezi kuna michezo mingi imefanyika,”amesema.
Amesisitiza kuwa hatua hiyo ni kuonesha ujumbe kwa jamii kwamba michezo ni sehemu muhimu kujilinda na magonjwa yasiyoambukiza na wanawaimarisha wafanyakazi wao waendelee kufanya michezo.

Dk Kisenge amefafanua kuwa mipango yao baada ya miaka 10 ni kwenda kufanya upandikizaji wa moyo,upasuaji wa tundu dogo,upasuaji kutumia roboti na kuongeza matawi sehemu mbalimbali za nchi na tutashirikiana na hospitali tofauti kutoa huduma.
“Sasa tunatawi Dar Group,Kawe,Arusha na Chato,tumeweka maabara kubwa imeshakamilika inafanya vitu mbalimbali na ndio maabara kubwa Afrika Mashariki na Kati .
Kuhusu gharama ya matibabu amesema bima ya afya kwa wote itakuwa suluhu hivyo anaomba wananchi wajitokeze kujiunga na bima.
“Tumeshirikisha wadau mbalimbali mwaka jana tulichangia bilioni 2.5 kwa ajili ya kusaidia matibabu ya watoto.Ninaomba wadau mbalimbali waendelee kutoa michango yao niishukuru serikali kwa asilimia 70 inalipia gharama za matibabu,”amefafanua.
Kwa upande wake Mwenyekiti kamati ya Bonaza ,Dk Evarest Nyawawa ameesema wameshirikiana na majirani zao kutoka hospitali ya Taifa ya Muhimbili,taasisi ya Tiba ya Mifupa (MOI),Chuki Kikuu cha Afya na Sayansi Kishiriki (MUHAS) na katika matawi yao.
“Tunasisitiza michezo ni sehemu ya kulinda afya ni tiba kabla ya matibabu tulikuwa na michezo ya mpira ,Michezo kukimbi,kukimbiza kuku,kuvuta kamba na netball .
Kapten wa timu ya mpira wa netball JKCI, Mariam Jumanne amesema katika mchezo huo wamecheza na MOI na wameibuka washindi kwa mabao 13 kwa 19 .
“Tunafuraha kupata ushindi huu kwenye michezo wowote siri ni mazoezi tumejitoa na tumefanya mazoezi tunahamasisha michezo kujikinga na magonjwa yasiyoambukiza sio tu michezo hii hata kukimbia ,”amesisitiza.



