Dk. Mwinyi asema ahadi za serikali zinatekelezwa

ZANZIBAR : MGOMBEA urais wa Zanzibar kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk Hussein Mwinyi amewatoa wasiwasi Watanzania juu ya kutekeleza ahadi inazonadi chama hicho katika kampeni zake.

Akizungumza kwenye Uwanja wa Hamburu Nungwi jana wakati wa mkutano wa kampeni wa mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, Dk Mwinyi alisema ahadi zote wa[1]nazoahidi zitatekelezwa kama ilivyokuwa kwenye ilani yao ya uchaguzi wa mwaka 2020-2025.

“Tulinadi ilani ya 2020 tulitekeleza na tena kuna sekta nyingine tumevuka,hakuna sababu hata moja ya kuwa na wasiwasi kwamba tunayoahidi hatutatekeleza, tukiahidi tunatekeleza nilisema yajayo yanafurahisha, sasa nasema yajayo ni neema tupu,”alisema Dk Mwinyi.

Aidha, Dk Mwinyi alihamasisha wananchi wa Zanzibar kudumisha amani, umoja,mshikamano na maridhiano kwani ndio sera ya nchi inavyotaka. “Bila amani hakuna maendeleo, msingi wa maendeleo wa nchi yoyote ni amani, nawaomba wagombea ubunge, udiwani,uwakilishi kila mmoja azungumze amani, hili ni jambo la msingi kabisa mengine yote yanakuja baadaye,” alisema.

Alitoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi kupiga kura siku ya uchaguzi. “Wingi huu na hamasa hii ionekane siku ya kupiga kura pia,” alisema. SOMA: Vyama vyampa ‘tano’ Dk Mwinyi ongezeko pensheni

Naye Katibu Mkuu wa CCM, Dk Asha-Rose Migiro aliwasifu wagombea urais hao Samia na Dk Mwinyi kwa kuulinda Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. “Tanzania ndio pekee yenye Muungano wa aina yake na CCM ndio inasimamia na kuuboreshmuungano umeimarika sana kiuchumi chini ya Samia,” alisema.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button