Masoud afanya kampeni soko la darajani

UNGUJA, Zanzibar: MGOMBEA Urais wa Chama cha ACT Wazalendo, Othman Masoud Othman, Sept 20, 2025 amefanya matembezi katika maeneo mbalimbali ya Soko la Darajani, Mjini Unguja, ikiwa ni sehemu ya kampeni zake kuelekea Uchaguzi Mkuu.
Katika ziara hiyo, Othman amekutana ana kwa ana na wafanyabiashara, akinamama na vijana, akisikiliza changamoto zao na kueleza mwelekeo wa Serikali ya ACT Wazalendo endapo itapewa ridhaa ya kuongoza Zanzibar. SOMA: ACT Wazalendo kuruhusu karafuu iuzwe popote
Soko la Darajani ni kitovu cha shughuli za kiuchumi kwa wananchi wengi wa Zanzibar, na kwa mujibu wa ACT Wazalendo, ziara ya mgombea wao katika eneo hilo inabeba ujumbe wa dhamira ya chama kujenga uchumi imara unaotokana na wananchi wenyewe.
 
				 
					



