Mbambabay mguu sawa kumpokea Samia

WANANCHI wa Wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma wameonesha shauku ya kusikiliza sera za mgombea wa kiti cha rais kupitia Chama cha Mapinduzi(CCM), Samia Suluhu HassanĀ ambaye leo ameanza mikutano ya kampeni katika majimbo ya mkoa huo
Mama lishe, Justine Haule amemshukuru Samia kwa kuendelea kutoa mikopo isiyo na tiba kwa wajasiriamali wakiwemo mama lishe. “Kwa kweli nataka kumuona shujaa wetu Mheshimiwa Samia, ni mama ambaye amejua kutukomboa wanawake kwa kutuwezesha mikopo isiyo na riba, ninaamini leo pia atatupa neno la matumaini, kwa kweli kura yangu ni ya Samia.”
Naye Pius George dereva amesema serikali imeimarisha miundombinu ya barabara hatua ambayo inawafanya biashara ya usafirishaji kuwa nzuri kwao. “Siku za nyumba ilikuwa barabara ilikuwa ni shida, lakini sasa mkeka umetulia mambo kwetu ni mazuri, tunachosubiri ni ifike Oktoba ili nitiki kwa Samia.” SOMA: Dk Samia kuitikisa Pemba kampeni leo



