RC Makalla aagiza kasi mradi wa maji Karatu

ARUSHA : MKUU wa Mkoa wa Arusha, CPA Amos Gabriel Makalla, ameagiza Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Karatu kuongeza kasi ya kumpata mkandarasi atakayeharakisha usambazaji wa maji kwa wananchi kutoka kwenye chanzo cha bwawani.

Akizungumza Septemba 22, 2025 wakati wa ziara yake mjini Karatu, Makalla alikagua chanzo hicho cha maji ambacho kiliharibiwa na mafuriko na kuathiri upatikanaji wa maji. Serikali imetenga fedha ili kukinusuru chanzo hicho muhimu kwa mji wa Karatu na maeneo jirani. SOMA: Mradi wa maji kunufaisha wananchi wa Mutukula

Makalla aliipongeza mamlaka hiyo kwa kufikisha huduma ya maji kwa asilimia 71 wilayani humo, lakini akasisitiza umuhimu wa kushirikisha jamii katika kulinda na kutunza vyanzo vya maji. “Niwasihi tushirikiane na wananchi kuhakikisha tunalinda vyanzo vya maji na kuendelea kutoa elimu kuhusu matumizi bora bila kuvichafua,” alisema Makalla.

Awali, Meneja wa Mamlaka ya Maji Karatu, Injinia Steven Siayi, alisema serikali imetoa zaidi ya Shilingi milioni 145 kwa ajili ya kupeleka maji kwenye tenki lenye ujazo wa lita 225,000, ambapo kisima hicho kina uwezo wa kuzalisha lita 28,000 kwa saa.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button