Chaumma: Bima ya afya, vyeti vya kuzaliwa bure

ARUSHA : CHAMA cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA) kimesema ndani ya siku 100 tangu kuingia madarakani kitawapa bure wananchi bima ya afya na vyeti vya kuzaliwa.
Mgombea mwenza wa urais kwa tiketi ya chama hicho, Devotha Minja alitoa ahadi hiyo kwenye mikutano ya kampeni katika majimbo ya Arumeru Magharibi na Mashariki. Minja alifanya mikutano katika kata za Ngaramtoni na Olturumet, Jimbo la Arumeru Magharibi na Usa Sokoni kwenye Jimbo la Arumeru Mashariki.
Pia, alisema Chaumma imejipanga ili ndani ya siku 100 wanawake wajawazito wasibebe mabegi ya nguo wakati wanakwenda kujifungua hospitali. Minja alisema serikali ya Chaumma haioni sababu za msingi za mwananchi kulipia bima ya afya au cheti cha kuzaliwa. Hivyo, watapata huduma hizo bure na kudai kuwa chama hicho kimejipanga kuwakomboa Watanzania.
Alisema mgombea urais kwa tiketi ya Chaumma, Salum Mwalimu ana mipango mingi ya kumkomboa Mtanzania, hivyo akaomba Oktoba 29, mwaka huu wananchi wamchague aiongoze nchi. SOMA: Chaumma yaahidi mambo matano siku 100 Ikulu
Naye Mgombea ubunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki kupitia Chaumma, Jackiline Kimambo alidai kuwa anatosha kuwa mbunge wa jimbo hilo akidai kuwa anafahamu changamoto zote zinazowakabili wananchi jimboni humo. Kimambo aliomba wananchi waache kupiga kura kwa mazoea akidai kuwa changamoto zinatatuliwa kwa mipango na mikakati na kitu hicho anayekiweza ni yeye.
“Nipeni ubunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki, ninajua kwa kina changamoto za jimbo hili na hakuna wa kuzitatua, ni mimi na hao walioongoza jimbo hili kwa miaka nenda rudi hawajafanya mabadiliko.
JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… You can earn from 6000-12000 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good earning opportunity. tab for more detail thank you……..
HERE——————————————⊃⫸ http://Www.Cash43.Com