Mkutano wa dharura DRC kufanyika Paris

DR CONGO : RAIS wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Felix Tshisekedi, amewaomba wanachama wa Umoja wa Mataifa kutambua mauaji ya kimya kimya nchini DR Congo. Kauli hiyo inafuatia kwa tangazo la Ufaransa kuwa itakuwa mwenyeji wa mkutano wa dharura kuhusu mzozo wa DR Congo mwezi ujao.
Akizungumza katika mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, Tshisekedi amesema vita nchini mwake vimeathiri wananchi kwa zaidi ya miaka thelathini. Ameomba tume huru ya kimataifa ya uchunguzi kusaidia kutafuta suluhisho la kiini cha mzozo wa mashariki mwa DR Congo.
Kwa upande wake, Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron, amesema mkutano huo utawaleta pamoja wale wote wanaoweza kushughulikia dharura za kibinadamu na kuchangia katika juhudi na mipango ya amani ambayo tayari inaendelea. SOMA: DRC : Spika wa bunge ajiuzulu