China yajipanga kudhibiti uchafu wa mazingira

BEIJING : CHINA, taifa linaloongoza kwa uzalishaji wa gesi chafu duniani, limetangaza kwa mara ya kwanza malengo ya kupunguza hewa zinazochochea ongezeko la joto duniani.
Tangazo hilo lilitolewa kwa njia ya video na Rais Xi Jinping katika mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu mabadiliko ya tabianchi, ambapo zaidi ya mataifa 120 yanawasilisha mikakati ya kudhibiti ongezeko la joto linalosababisha majanga kama mafuriko na moto wa nyika.
Kwa mujibu wa mpango huo, China inalenga kupunguza uzalishaji wa gesi chafu kwa asilimia 7 hadi 10 ifikapo mwaka 2035. SOMA: PURA yaipongeza TPDC gesi asilia katika uchumi
Wachambuzi wamesema ingawa kiwango hicho kinaweza kuonekana kuwa kidogo, China ina historia ya kuweka malengo ya chini lakini kuyatimiza kwa kiwango kikubwa, hasa kwa kuwekeza kwenye teknolojia rafiki kwa mazingira.