Mbaroni kwa kukwepa kodi ya bil 2.5/-

IRINGA: Mfanyabiashara wa mbao kutoka Mafinga, Mosses John Madege, mwenye usajili wa TIN namba 130299024, anadaiwa kukwepa kodi ya Sh Bilioni 2.5 na sasa anakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi namba 23655/2025, iliyosomwa kwa mara ya kwanza leo katika Mahakama ya Mkoa wa Iringa.
Mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Japhet Bwire Manyama, mawakili wa serikali wakiongozwa na Medalakini Emmanuel wakisaidiana na Auni Chilamula walisoma mashtaka 25 dhidi ya Madege.
Kwa mujibu wa upande wa mashtaka, kati ya mwaka 2022 hadi 2024 mtuhumiwa aliwasilisha ritani za Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) zenye taarifa za uongo, kinyume na kifungu cha 84(1) cha Sheria ya Usimamizi wa Kodi.
Inadaiwa alionyesha kufanya manunuzi kutoka kwa wafanyabiashara mbalimbali kupitia mfumo wa malipo kwa taasisi za umma (GPG), ilhali taarifa hizo hazikuwa za kweli.
Vitendo hivyo vinahusisha makosa 23 ya awali, na kupelekea kosa la 24 la kukwepa kodi kwa njia ya udanganyifu.
Kosa la mwisho, la 25, ni uhujumu uchumi kwa kusababisha hasara kwa Mamlaka ya Mapato kutokana na kodi ambayo haikulipwa kufuatia taarifa za uongo.
Madege alifikishwa mahakamani na Idara ya Upelelezi wa Kodi Kanda ya Nyanda za Juu Kusini.
Hata hivyo, licha ya kupewa masharti ya dhamana, ikiwemo kuweka nusu ya fedha za hasara iliyosababishwa, alishindwa kutimiza masharti hayo na kurejeshwa mahabusu.
Akizungumza baada ya kesi, Meneja wa Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Nicolous Njovu, alisema mtuhumiwa huyo amekwepa kodi ya Sh Bilioni 2.5.
Kwa upande wake, Meneja wa TRA Mkoa wa Iringa, Peter Jackson, alisema hatua hiyo itakuwa fundisho kwa wafanyabiashara wengine wenye tabia ya kukwepa kodi, huku ikisaidia kuimarisha usawa na mazingira bora ya biashara.
Kesi hiyo imepangwa kutajwa tena Oktoba 1, mwaka huu.
Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
.
More Details For Us→→→→→→→→→→ http://Www.Payathome9.Com
JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… You can earn from 6000-12700 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good earning opportunity. tab for more detail thank you……..
.
This is my main concern……………………………………. http://Www.Cash43.Com