Rais Samia afanya uteuzi DART

DAR ES SALAAM: Rais Dk. Samia Suluhu Hassan amemteua, Said Habibu Tunda kuwa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) akichukuwa nafasi ya Dk Athumani Kihamia ambaye uteuzi wake umetenguliwa.
Aidha, taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Sharifa Nyanga, imeeleza kuwa Pius Andrew Ng’ingo ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Mabasi Yaendayo Haraka (UDART). Ng’ingo anachukua nafasi ya Waziri Kindamba ambaye uteuzi wake umetenguliwa. Uteuzi huo unaanza mara moja.



