Vyama vya siasa kujadili Katiba mpya

DAR –ES-SALAAM : VYAMA vikuu vya siasa nchini vimeweka upatikanaji wa Katiba Mpya kama kipaumbele katika ilani zao kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu, hatua ambayo imeibua matumaini mapya ya kufufua mchakato huo uliochukua zaidi ya muongo mmoja bila mafanikio.
Hayo yamesemwa Dar es Salaam na Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu (THRDC) wakati wakitoa uchambuzi wa ilani za vyama vya siasa kuhusu Katiba Mpya na mapendekezo ya Asasi za Kiraia (AZAKI) kuhusu uhuishaji wa mchakato huo.
Mtandao huo umesema kwa kuwa kila chama kimeweka kama kipaumbele sasa ni wakati wa taifa kurejea kwenye ajenda hiyo muhimu ya kitaifa. Katika ilani hizo, ACT Wazalendo imeahidi kukamilisha mchakato wa Katiba ndani ya mwaka mmoja, huku CHAUMMA ikiahidi kuwasilisha muswada wa sheria ya Katiba Mpya bungeni ndani ya siku 100 baada ya kuunda serikali.

CUF imeeleza kuwa itaanza mjadala wa kitaifa wa Rasimu ya Warioba ndani ya miezi mitatu, wakati CCM kupitia mgombea wake Dk Samia Suluhu Hassan, imeahidi kuhuisha mchakato huo ndani ya siku 100 za kwanza. THRDC imesema ahadi hizo ni ishara ya mwanga mpya kwa mustakabali wa taifa, lakini umesisitiza umuhimu wa kuzifuatilia kwa karibu ili kuhakikisha wananchi wanapata Katiba Mpya yenye misingi ya maridhiano ya kitaifa.
Akizungumza kwenye kikao hicho na waandishi wa habari, Mkurugenzi wa Programu wa THRDC, Halima Sonda, alisema mashirika ya kiraia kupitia Ilani ya “Tanzania Tuitakayo” yameendelea kushinikiza ajenda ya Katiba Mpya kuwa sehemu ya vipaumbele vya kitaifa sambamba na haki za binadamu, utawala bora na huduma bora za jamii.
Kwa upande wake, Mkuu wa Idara ya Utetezi wa THRDC, Wakili Paul Kisabo, alitoa historia ya Katiba nchini kuanzia Katiba ya Uhuru ya mwaka 1961 hadi Katiba ya sasa ya mwaka 1977 ambayo imefanyiwa mabadiliko mara 14, akibainisha kuwa bado haijawahi kupata mwafaka mpana wa kitaifa.
Mratibu wa Taifa wa THRDC, Wakili Onesmo Olengumwa, alisema mchakato wa Katiba Mpya uliokwamia mwaka 2014 ulitokana na mgawanyiko wa kisiasa, ukosefu wa utashi wa kisiasa na ukaribu na Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015, hivyo akasisitiza haja ya kujifunza kutokana na changamoto hizo.
Olengumwa alisema AZAKI zinaamini muda huu ni sahihi zaidi kurejea kwenye ajenda ya Katiba kwa kuwa vyama vingi vya siasa vimeonesha dhamira ya kisiasa kupitia ilani zao. “Tunapaswa kuhakikisha wananchi wanashiriki kikamilifu, na mchakato huu hauchukuliwi kwa mtazamo wa ushindani wa vyama, bali mustakabali wa taifa,” alisema.
Mashirika hayo yamependekeza hatua za kuhakikisha safari ya Katiba Mpya inafanikiwa, ikiwemo kuanzishwa kwa mwafaka wa kitaifa, kushirikisha wananchi ipasavyo, kuwepo kwa dhamira ya kisiasa thabiti na kuepusha mchakato kufanyika karibu na uchaguzi. Vilevile, yamesisitiza haja ya uwazi, uwajibikaji wa tume zitakazoundwa na kuangalia mifano ya nchi jirani kama Kenya na Afrika Kusini zilizofanikiwa kutengeneza katiba shirikishi.
Wadau hao wamesema jukumu kubwa liko kwa viongozi wa kisiasa kutafsiri ahadi zao katika vitendo, ili taifa lipate Katiba Mpya inayojenga umoja, haki na ustawi wa Watanzania wote. SOMA: CCM yajipanga mchakato katiba mpya




I get paid over (90$ to 500$ / hour ) working from home with 2 kids at home. I never thought I would be able to do it but my best friend earns over $22000 a month doing this and she convinced me to try. it was all true and has totally changed my life… This is what I do, check it out by Visiting Following web….
.
HERE——————————————⊃⫸ http://Www.Cash43.Com
Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
.
More Details For Us→→→→→→→→→→ http://Www.Payathome9.Com