Samia: Tunamuenzi baba wa Taifa kwa utawala bora

MGOMBEA urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema chama hicho kimeendelea kumuenzi Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, kwa kuendeleza misingi ya utawala bora unaojali utu na maslahi ya kila Mtanzania.
Dk. Samia ametoa kauli hiyo leo, Oktoba 10, wakati akihutubia wananchi wa Butiama, mkoani Mara, ikiwa ni muendelezo wa kampeni zake kuelekea uchaguzi mkuu wa Oktoba 29, ambapo ameeleza kuwa CCM bado inaenzi na kuendeleza misingi aliyoweka Mwalimu Nyerere tangu kuasisiwa kwa Taifa. “Katika kumuenzi Hayati Mwalimu Nyerere, hatuwezi kumtenganisha na misingi ya kiitikadi na kifalsafa aliyoijenga”. SOMA: Wasira asifu uhodari, uwezo wa Dk Samia



