Kikwete aibuka, asema sijakufa, nipo salama

RAIS Mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete amebainisha kuwa kitendo cha kuanika ukweli kuhusu maendeleo makubwa yaliyofanywa na Serikali chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan, ndiyo yamewafanya baadhi ya watu kusema maneno ya ajabu, ikiwemo kudai kuwa yeye amekufa au anapaswa kupumzika.

Hata hivyo, Kikwete amebainisha hadharani  kwamba hajafa, haugui popote na wala hajaamka na kichomi na kwamba wale wote wanaomuombea mabaya watakufa wao yeye ndio atakayeenda kuwazika. Akizungumza katika mkutano wa kampeni uliofanyika mjini Bagamoyo, mkoani Pwani, Kikwete alisema baadhi ya watu wanadhani kwa sababu anazungumza kuhusu mafanikio makubwa ya CCM, basi labda amechoka kisiasa au amekufa jambo ambalo alisema si kweli hata kidogo.

“Mimi ninasema kwa haya maendeleo yanayoonekana chini ya CCM chama hiki kitaendelea kuchaguliwa, sasa nikiyasema haya kuna wengine wanasema huyu mzee apumzike wengine kafa. Nawaambia mimi mzima wa afya njema. Wanaosema nimekufa, watakufa wao na mimi nitaenda kuwazika,” alisema.

Alisema katika kipindi cha miaka minne na nusu ya uongozi wa Rais Samia, Tanzania imepiga hatua kubwa katika nyanja mbalimbali zikiwemo miundombinu, afya, elimu, nishati, utalii na uchumi kwa ujumla. SOMA: Tuache chokochoko tudumishe amani

 

Habari Zifananazo

3 Comments

  1. Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
    .
    M­­­­­­o­­­­­­r­­­­­­e­ D­­­­­­e­­­­­­t­­­­­­a­­­­­­i­­­­­­l­­­­­­s For Us→→→→ http://Www.Payathome9.Com

  2. Start now making every month extra $19k or more by just doing an easy online job from home. Last month I earned and received $16650 from this job by giving only 3 hrs. a day. Every person can now get this job and start earning online by:-

    Open This…. http://Www.Work99.Site

  3. JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… You can earn from 6000-12700 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good earning opportunity. tab for more detail thank you……..
    .
    This is my main concern……………………………………. http://Www.Cash43.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button