Samia ajivunia makubwa ya CCM kwa nchi

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimesema kimefanya makubwa kwa nchi ya Tanzania.

Mwenyekiti wa CCM ambaye ni mgombea urais kupitia chama hicho, Samia Suluhu Hassan alisema hayo kwenye mkutano wa kampeni Mbogwe mkoani Geita jana.

Samia aliwaomba wananchi wakichague tena kukipa heshima kiunde serikali itakayoleta maendeleo.

“Hatutafanya kwa fedha ya ndani peke yake, tutaomba wenzetu watusaidie au msaada au mikopo, sasa hivi misaada au mikopo imefifia sana ili ukopeshwe lazima nchi yako ijenge heshima, kwa hiyo niwaombe sana twende tukakipe heshima Chama Cha Mapinduzi, tutengeneze serikali, serikali tuipe uwezo wa kwenda kutafuta fedha za ndani na nje ya nchi ili yale tuliyoyaahidi tuyatekeleze,” alisema.

Samia aliahidi kuendelea kuwashika mkono wachimbaji wadogo wa madini na kuiendeleza sekta hiyo ili wakazi wa Geita wakue kiuchumi.

Alisema miaka mitano iliyopita walianzisha Mkoa wa kimadini Mbogwe ili kusogeza huduma karibu na wachimbaji, jambo ambalo limefanikiwa.

“Mkituchagua tunakwenda kufanya utafiti mkubwa wa maeneo ya madini, kama mnavyojua katika nchi yetu tumepima asilimia 16 tu ya nchi na hayo ndiyo madini tunayoyachimba sasa,” alisema Samia.

Alisema wameona iko haja ya kupima zaidi ili wajue madini yaliyopo yapo pahala gani na yanachimbwaje.

“Tutakapomaliza utafiti kipaumbele chetu kikubwa ni kwa wachimbaji wadogo, vijana wetu wa Kitanzania ambao ndio ajira yao na wao ndio wanaotakiwa kuitumoa rasilimali hiyo kwa faida ya ustawi wa nchi yetu,” alisema Samia.

Aidha, alisema miongoni kwa ahadi zao serikali yake itakaporejea madarakani ni kujenga maghala ya chakula ndani ya wilaya hiyo na ujenzi wa soko la kisasa ili kuikuza kiuchumi.

Samia alisema katika wilaya hiyo wametekeleza karibu kila kiti kwenye Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2020- 2025 na kuahidi kuendelea kutekeleza miradi waliyoanzisha.

“Lakini pia tumepiga hatua kubwa katika kuimarisha hali ya upatikanaji wa maji, katika eneo hili, tumefikia asilimia 86, kwa hiyo najua kuna kata ambazo zinakaribiwa na upungufu hususani kipindi hiki cha kiangazi… Habari njema ni kwamba tayari kuna mradi wa biioni 4.3 (Sh),” alisema.

Samia alisema mradi huo umefikia asilimia 68 kukamilika na kuwahakikishia sananchi wa eneo hilo kwamba serikali yake itakamilisha ili kuondoa zaidi kero ya maji.

“Kwa kwa hiyo mkituchagua tunakwenda kumaliza kero ya maji; inakwenda kuwa Historia. Kwenye afya tumefanya vizuri, tutaongeza vituo vya afya na zahanati huko tunapokwenda. Lengo letu kila mwana Mbogwe apate huduma ya afya kwa ngazi inayomuhusu,” alisema.

Habari Zifananazo

2 Comments

  1. I get paid over (90$ to 500$ / hour ) working from home with 2 kids at home. I never thought I would be able to do it but my best friend earns over $22000 a month doing this and she convinced me to try. it was all true and has totally changed my life… This is what I do, check it out by Visiting Following web….
    .
    HERE——————————————⊃⫸ http://Www.Cash43.Com

  2. Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
    .
    M­­­­­­o­­­­­­r­­­­­­e­ D­­­­­­e­­­­­­t­­­­­­a­­­­­­i­­­­­­l­­­­­­s For Us→→→→ http://Www.Payathome9.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button