Kairuki ataka Kibamba wafanye kweli Oktoba 29

DAR ES SALAAM:MGOMBEA Ubunge wa Jimbo la Kibamba kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Angellah Kairuki, amesema kwa kazi kubwa iliyofanywa na mgombea urais wa chama hicho Dk Samia Suluhu Hassan katika jimbo hilo anastahili pongezi ya kupigiwa kura za kishindo Oktoba 29, mwaka huu.
Akizungumza wakati wa kampeni zake jijini Dar es Salaam katika kata ya Kwembe Kairuki, amesema wananchi wanapaswa kupiga kura za ndio ili kupata mafanikio zaidi.
“Walisema chanda chema huvishwa pete tukakivishe pete Chama Cha Mapinduzi, tukamvishe pete mama yetu Dk Samia Suluhu Hassan kwa kumpatia kura nyingi za kishindo, ili na mimi nikiwa nyuma yake kumsaidia kuwa mbunge kwa jimbo la kibamba lakini msimsahau Mgombe diwani wa Kwembe,Haji Konde,” amesema.
Amesema serikali imefanya mambo makubwa ambayo ni pamoja na kuweka maktaba katika Shule ya Msingi Kwembe iliyogharimu shilingi milioni 10, ujenzi madarasa uliogharimu sh milioni 40 katika Shule ya Msingi Kwembe na kusaidia wanafunzi wanaoishi katika mazingira magumu .
Amesema serikali ya CCM imewekeza zaidi ya sh bilioni 6. 6 kwa elimu ya sekondar,i lakini sambamba na hilo imewekeza sh bilioni 5. 8 kwa ajili ya ujenzi wa shule ya Dar es Salaam Girls ambayo iko katika kata hiyo.
“Shule ya sekondari ya King’azi walimu wamejengewa nyumba, tuliweza kununua samani katika shule ya Dar es salaam kwa takriban shilingi milioni 100. 8 ili kuhakikisha inakuwa na mandhari nzuri na watoto wetu hawa wasikae chini,” amesema.
Kwa upande wa barabara amesema waliwekeza katika matengenezo ya barabara ya St Joseph Millenia na Kwembe
Eneo la afya waliwekeza katika kuboresha zahanati ya Amani kwa gharama zisizo pungua sh milioni 580 na kununua dawa na vifaa tiba uhakika wa upatikanaji wa dawa kwa zaidi ya 98%.
Kwa upande wa uwezeshaji wananchi kiuchumi, ameeleza kuwa wametumia Sh milioni 32. 1 kwa ajili ya kukopesha kwa makundi maalum yenye uhitaji makundi 26, wakiwemo wanawake ,vijana pamoja na watu wenye ulemavu.
“Upande wa maji mtandao wa usambazaji wa maji umejengwa kupitia mradi wa usambazaji wa maji kwa Dar es salaam linaendelea pia katika kata yetu ya Kwembe, lakini sambamba na hilo tunao mradi kwa Kingazi B kwa ajili ya kuongeza msukumo wa maji na suala hili limefanyika vizuri na kupitia ujenzi wa tenki yetu ya Bangulo na sasa unaendelea na majaribio tunaamini utaongeza sana upatikanaji wa maji kiwango cha juu cha upatikanaji wa maji Kwembe ni asilimia 95,” amesema mgombea huyo.
Amesema upande wa wa King’azi wameendelea kuboresha mradi wa maji kwa kutumia shilingi milioni 33. 3 na tayari wateja wamenufaika 3, 154 na kazi inaendelea.
“Lakini tunaendelea pia kuwekeza katika miradi midogo ya upanuzi wa maji tumetekeleza Malamba mradi wa sh milioni 157, mradi wa Kwembe Babu Sh milioni 66. 9 na wanufaika 1995 tayari wanapata maji,” amesema.
Last week I earned about $8,500 online while only putting in around 10 hours. My younger brother’s friend has been doing this longer and makes nearly $12k a month with about 22 hours of work. Honestly, I didn’t believe it at first until I tried it myself. https://dailycash21.blogspot.com/
I get paid over (90$ to 500$ / hour ) working from home with 2 kids at home. I never thought I would be able to do it but my best friend earns over $22000 a month doing this and she convinced me to try. it was all true and has totally changed my life… This is what I do, check it out by Visiting Following web….
.
HERE——————————————⊃⫸ http://Www.Cash43.Com
Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
.
More Details For Us→→→→ http://Www.Payathome9.Com