Dk. Samia kusaka kura za CCM Kagera

MGOMBEA Urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Samia Suluhu Hassan, anatarajiwa kufanya ziara ya kampeni mkoani Kagera tarehe 15 na 16 Oktoba mwaka huu, kwa ajili ya kuomba kura za wananchi wa mkoa huo katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2025–2030.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Bukoba, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kagera, Nazri Karamagi, alisema kuwa mgombea huyo ataanza ziara yake tarehe 15 Oktoba kwa kufanya mikutano mitatu ya kampeni katika wilaya za Muleba, Missenyi na Karagwe.
Karamagi alisema kuwa tarehe 16 Oktoba, Mama Samia atahitimisha ziara yake kwa kufanya mkutano mkubwa wa hadhara katika Uwanja wa Kaitaba, Bukoba Mjini, ambapo ataomba ridhaa ya wananchi na kuwaombea kura wagombea ubunge na udiwani wa CCM mkoani humo. SOMA: Samia: Nimemuenzi Magufuli
Alitoa wito kwa wananchi wa Kagera kujitokeza kwa wingi kumsikiliza mgombea huyo na kufahamu sera pamoja na Ilani ya CCM kwa miaka mitano ijayo. “Tunajua Mama Samia amefika Kagera mara nyingi akiwa Rais, lakini safari hii anakuja kama mgombea. Ni muhimu wananchi wakasikiliza sera na mipango ya chama, pamoja na mafanikio yaliyopatikana katika kipindi chake cha uongozi,” alisema Karamagi.
Kutokana na ujio huo, hamasa imeongezeka katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Kagera, hasa mjini Bukoba, ambapo viongozi wa chama, wagombea na mabalozi wa mashina wameendelea kuhamasisha wananchi kujitokeza kwa wingi Uwanjani Kaitaba kumsikiliza mgombea huyo wa CCM.
Make money while staying at home and working online. I just received $23,783 for my work last month, and I was doing this part-time. This year, I plan to earn even more, and I believe you can also make extra cash from this job. To join right now, follow the details on this website.
Open This… http://Www.Work99.Site
Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
.
More Details For Us→→→→ http://Www.Payathome9.Com