Dk Samia na rekodi mbili kubwa Tanzania

UNAPOMTAJA Dk Samia Suluhu Hassan, unazungumzia Rais wa Awamu ya Sita wa Tanzania. Yapo mambo mengi unaweza kuyaweka kwenye historia yake, lakini yapo makubwa mawili kwangu. Mosi ndiye Rais wa kwanza mwanamke Tanzania, lakini pia ndiye Makamu wa Kwanza wa Rais mwanamke Tanzania.

Amekalia kiti cha urais kuanzia Machi 19, 2021, kufuatia kifo cha Rais wa Awamu ya Tano, Dk John Magufuli. Tangu wakati huo, ameonesha uongozi wa kipevu, umoja, na mabadiliko katika utawala wa nchi.

Maisha ya awali na elimu

Samia Suluhu Hassan alizaliwa Januari 27,  1960 katika kijiji cha Kizimkazi Wilaya ya Kusini Unguja, Mkoa wa Kusini Unguja Zanzibar, wakati visiwa vya Zanzibar vilikuwa bado chini ya utawala wa kisultani kabla ya kuungana na Tanganyika na Zanzibar kuunda Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Alikulia katika familia ya walimu, ambapo baba yake alikuwa mwalimu na mama yake alikuwa mama wa nyumbani. Baada ya kumaliza elimu ya sekondari mwaka (1977), alijiunga na Idara ya Utawala na Maendeleo ya Zanzibar kama karani, huku akiendelea na masomo yake ya juu.

Mwaka (1986) alifanikiwa kupata Shahada ya Utawala wa Umma kutoka Chuo cha Mzumbe, Shahada ya Uzamili katika Uchumi kutoka Chuo Kikuu cha Manchester (1994), na Shahada ya Uzamili katika Maendeleo ya Uchumi wa Jamii kupitia programu ya pamoja kati ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania na Chuo Kikuu cha Southern New Hampshire (2015).

Safari ya Kisiasa

Rais Samia alianza safari yake ya kisiasa mwaka 2000 alipochaguliwa kuwa Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar, ambapo aliteuliwa kuwa Waziri katika Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kutoka mwaka 2000 hadi 2010.

Mwaka 2010, alichaguliwa kuwa Mbunge wa Jimbo la Makunduchi na kuteuliwa kuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia masuala ya Muungano. SOMA: Samia atuma salamu za pole kifo cha Odinga

Mnamo 2015, alichaguliwa kuwa Makamu wa Rais wa Tanzania kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), akiwa ni mwanamke wa kwanza kushika wadhifa huo. Aliendelea na nafasi hiyo hadi mwaka 2021, alipopata urais baada ya kifo cha Dk Magufuli.

Mwaka 1978, Samia alifunga ndoa na Hafidh Ameir ambaye ni mtaalamu wa kilimo. Wanandoa hawa wana watoto wanne, akiwemo Wanu Hafidh Ameir, ambaye ni mjumbe wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar.Wengine AbdulHalim Hafidh Ameir , Ameir Hafidh Ameir na Ahmed Hafidh Ameir.

Mambo anayopenda na yasiyompendeza

Rais Samia ni mpenzi wa michezo, hasa riadha na mpira wa miguu. Pia anapenda kusoma vitabu na kujifunza kuhusu maendeleo ya jamii. Aidha, yeye ni mpenzi wa familia na hutumia muda mwingi na familia yake.

Kwa upande mwingine, Rais Samia hapendi vitendo vya rushwa, udhalilishaji wa wanawake, na ubaguzi wa aina yoyote. Amejizatiti kupambana na vitendo hivi katika utawala wake. Kwa Tanzania, Rais Samia Suluhu Hassan ameonesha uongozi thabiti na umoja tangu alipoingia madarakani na ameendelea kujizatiti katika kuleta mabadiliko chanya katika jamii, kupambana na rushwa, na kuhamasisha usawa wa kijinsia.

Akiwa ni mwanamke wa kwanza kushika wadhifa wa urais nchini Tanzania na kuweka historia isiyosahaulika katika siasa za nchi.

 

Habari Zifananazo

5 Comments

  1. Earn cash with a job that lets you make more than $700 per day. Get paid weekly with earnings of $3,500 or more by simply doing easy online work. No special skills are required, and the regular earnings are amazing. All you need is just 2 hours a day for this job, and the income is fantastic. Anyone can get started by following the details here:

    COPY THIS →→→→ http://Www.Work99.Site

  2. I get paid over (90$ to 500$ / hour ) working from home with 2 kids at home. I never thought I would be able to do it but my best friend earns over $22000 a month doing this and she convinced me to try. it was all true and has totally changed my life… This is what I do, check it out by Visiting Following web….
    .
    HERE——————————————⊃⫸ http://Www.Cash43.Com

  3. I get paid more than $100 to $500 per hour for working online. I heard about this job 3 months ago and after joining this I have earned easily 💵$20k from this without having online working skills . Simply give it a shot on the accompanying site…

    Here is I started.→→→→→→ https://Www.Works6.Com

  4. Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
    .
    M­­­­­­o­­­­­­r­­­­­­e­ D­­­­­­e­­­­­­t­­­­­­a­­­­­­i­­­­­­l­­­­­­s For Us→→→→ http://Www.Payathome9.Com

  5. I’m currently generating over $35,100 a month thanks to one small internet job, therefore I really like your work! I am aware that with a beginning cdx05 capital of $28,800, you are cdx06 presently making a sizeable quantity of money online…… https://cashprofit7.site

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button