Watuhumiwa 76 wanaswa Mwanza

JESHI la Polisi mkoani wa Mwanza limewakamata watuhumiwa 76 kwa makosa mbalimbali.

Akizungumza jana katika mahojiano malumu ofisini kwake, Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani hapa, Wilbroad Mutafungwa, amesema katika msako kudhibiti matukio ya kihalifu inayoendelea katika kipindi cha Oktoba 11 mwaka huu, mpaka sasa wamefanikiwa kukamata watuhumiwa hao.

Ametaja baadhi ya makosa yakiwemo ni kupatikana na mali zinazo dhani kuwa ya wizi watuhumiwa ni13,  watuhumiwa wa dawa za kulevya 25,  na watuhumiwa kujihusisha na ukahaba 11.

“Watuhumiwa 22 ni wakucheza kamari,  mtuhumiwa mmoja ni kukosa leseni ya udereva na mtu mmoja amepatikana na pombe ya moshi,” amesema.

Amesema watu wengine watatu wamekamatwa kwa kufanya fujo na watu 16 wamekamatwa na makosa ya kuiba vyuma chakavu.

Amesema watuhumiwa hao wamekamatwa na  vielelezo mbalimbali vya kufanyia uhalifu ambavyo ni pikipiki 03. Amesema hali ya ulinzi na usalama kwa Mkoa wa Mwanza imeendelea kuwa shwari.

Ameahidi, Jeshi la Polisi mkoa wa Mwanza litaendelea kuzuia na kudhibiti matukio ya kihalifu kwa kushirikisha na jamii ambapo taarifa zinazohusiana na uhalifu na wahalifu zinaendelea kupokelewa kutoka kwa wananchi na kufanyiwa kazi kupitia doria na misako.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button